1 Kings 5:2-6

2 aSulemani akapeleka ujumbe huu kwa Hiramu:

3 b“Unajua kwamba kwa sababu ya vita vilivyopiganwa dhidi ya baba yangu Daudi kutoka pande zote, hakuweza kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana Mwenyezi Mungu wake, hadi Bwana alipowaweka adui zake chini ya miguu yake. 4Lakini sasa Bwana Mwenyezi Mungu wangu amenipa utulivu kila upande hakuna adui wala maafa. 5 cKwa hiyo, ninakusudia kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana, Mungu wangu, kama Bwana alivyomwambia baba yangu Daudi, wakati aliposema, ‘Mwanao nitakayemweka kwenye kiti cha ufalme mahali pako, ndiye atajenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu.’

6

d“Hivyo toa amri ili mierezi ya Lebanoni ikatwe kwa ajili yangu. Watu wangu watafanya kazi na watu wako, nami nitawalipa watu wako kwa ujira wowote utakaoupanga. Unajua kwamba hatuna mtu yeyote mwenye ustadi katika kukata miti kama Wasidoni.”

Copyright information for SwhKC